4/15/2022

Mke Amlazimisha Mumewe Kuoa Mdada Msusi wa Mnywele

Kulingana na Taifa Leo, mke wa jamaa aliwaacha wengi midomo wazi alipotoa kauli hiyo iliyomshangaza mumewe.

“Usidhani mimi sijui mambo unayoendeleza kule mtaani, najua una mpango wa kando ndio maana huwa hautulii hapa nyumbani.

Kama hutosheki na mimi nakusihi uoe mwanamke mwingine na sitokuwa na shida, nitakubali kuwa mke mwenza,” kisura alimwambia jamaa.

Inaarifiwa kwamba jamaa alibaki amekodoa macho asijule la kutamka.

“Haiwezekani. Umejuaje nina mpamgo wa kando? Siwezi kuoa mke wa pili” lofa alisema.


Hata hivyo mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya mama kudai kwamba atamwacha lofa iwapo hangekubali kuoa mke wa pili.

Nairobi: Kijogoo Afumaniwa Akichovya Mizinga ya Vipusa Wawili
“Unayechepuka naye huko nje mimi namjua tena vizuri sana. Alikuwa rafiki yangu na ninamjua vizuri sana kukuliko. Heri umuoe kama unataka mambo yawe sawa katika hii nyumba. Sitaki uniletee magonjwa ya zinaa hapa kwa sababu ya uzinifu wako,” demu alisema.

Jamaa kwa upande wake aliwaza na kuwazua na baada ya hapo akadai hakuwa na uwezo wa kuishi na wanawake wawili.

“Siwezi kuishi na wanawake wawili. Ni wewe unanitosha tu,” jamaa alisema.o

“Kama huna uwezo wa kuishi na wanawake wawili unanipuuza kwa nini? Unashindana na nani kule nje kwa uzinifu? Fanya uamuzi wako haraka kabla sijachukua hatua,” kipusa alisema.

Hata hivyo, haikujulikana kilichojiri baada ya lofa kusukumwa na mkewe aoe mke wa pili ili asitishe tabia ya kuchepuka.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger