Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mlevi Azikwa Kwenye Jeneza la Chupa ya Bia, Alipenda KulewaHuko nchini Ghana kuna video inaendelea kusambaa mitandaoni ikimuonesha bwana mmoja akiwa kwenye jeneza lililoundwa kwa muonekano wa chupa ya bia.

Ingawa jina la mtu huyo halijawekwa wazi lakini inadaiwa mtu huyo alikuwa akipenda sana kunywa bia enzi za uhai wake na hivyo marafiki na jamaa zake katika kile wanachodai ni kumuenzi na kumuaga kwa heshima, wameamua kumtengenezea jeneza lenye mfanano na kile alichopenda kukinywa enzi za uhai wake.

Jeneza hilo linaelezwa kuundwa kwa aina ya bia moja maarufu nchini humo. Hata hivyo katika taifa la Ghana kumeripotiwa kuwa si jambo la kushangaza sana kutokana na wengi kuzikwa katika mitindo mbalimbali ya majeneza kulingana tu na kile hao waliotangulia walikuwa wanapenda nini ama wanajishughulisha na kitu gani.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments