Ticker

6/recent/ticker-posts

Mtendaji Serikali ya Mtaa Mbezi Msumi Achinjwa ofisini kwake
Watu wawili ambao hawajafahamika wamemchinja Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Msumi aliefahamika kwa Jina la Kelvin akiwa ofini kwake siku ya leo majira ya saa 8 mchana katika kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Taarifa kutoka kwa Shuhuda wa tukio hilo zinasema kuwa Mtendaji huyo alifika ofisini kama kawaida asubuhi na kuanza shughuli za kuhudumia wananchi na ilipofika mida ya saa 8 mchana majirani wa ofisi hiyo walishuhudia vijana wawili wakitoka kwa kasi kutoka ofisini kwa mtendaji huyo.

Baada ya kufuatilia wakakuta Mtendaji amechinjwa na shingo ikiwa Inaning’inia huku akiwa amekaa kwenye kiti chake na tayari alikua ameshafariki.

Baada ya Tukio hilo kujaza watu wengi na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo walipofika lilifika eneo la tukio wakiwa na waliondoka na Mwili wa Marehemu huku ofisi hiyo ikifungwa na watu wakiamuriwa kutawanyika.


 
Taarifa za awali hazijataja sababu za tukio hilo huku Dar 24Media ikiendelea kufuatilia undani wa Tukio Hilo na taarifa zaidi zitatolewa.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments