Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mtoto wa Mwaka Mmoja, Wengine Watatu Wafariki Ajali ya Gari

Mtoto mmoja wa mwaka mmoja na nusu na watu watatu wamefariki dunia baada ya gari dogo ya abiria inayofanya safari kati ya Kilwa Masoko na Nangurukuru mkoani Kilwa kugongana na uso kwa uso na gari mkurugenzi wa wilaya Kilwa.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, kamishna msaidizi  Mtatiro Kitinkwi,   amethibisha kutokea   kwa ajali hiyo  ambayo imehusisha  gari dogo la mkurungenzi wa kilwa  na gari ya aina ya probox  iliyobeba abiria  ambapo  watu wanne  wamefariki dunia wakiwamo  wanawake wawili, mwanaume mmoja na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijathibitishwa." Ni kweli kwamba watu wanne wamefariki  wakiwamo  mama wawili watu wazima , mwanaume mmoja mtu mzima na mtoto mmoja wenye umri wa mwaka mmoja na nusu  " amesema kamanda Kitinkwi.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments