Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwalimu wa Shule ya Msingi Afariki DUNIA Kwa Kufakamia Pombe Bila Kula


Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ameripotiwa kufariki dunia baada ya kunywa pombe za kienyeji bila ya kula.

Mwalimu huyo Sam Kadama wa shule ya msingi Chankhandwe iliyopo Lilongwe nchini Malawi, anadaiwa alikunywa pombe hiyo inayojulikana kwa jina la Kachasu muda mfupi mara baada ya kutoroka kazini.

Uchunguzi wa madaktari umebaini kuwa mwalimu huyo amefariki dunia kutokana na kunywa pombe hiyo ya kienyeji kupitiliza na akiwa hajala.

Polisi katika eneo la Sinyala kulipotokea mkasa huo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo tayari wameukabidhi mwili kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments