Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mwanamke jifunze namna ya kujiongezea thamani katika mahusiano yako
Wadada wengi hudanganyika na kujiona wako na mwanaume sahihi eti kwa sababu mwanaume huyo anampa pesa, anampeleka ku-enjoy maeneo ya gharama na kadharika..hizo sio sifa pekee za mwanaume sahihi!

Hebu subiri kidogo, je mwanaume huyo amewahi kukuuliza kuhusiana na career na ndoto zako?

Je matendo yake yana U-MUNGU ndani yake?, Je huwa anakuthamini muda wowote na sio anapotaka sex pekee? Je amewahi kukushirikisha walahu robo tatu ya vision(maono) yake na kuhitaji mawazo yako?

Je anakukumbuka kimawasiliano au inapita hata siku nzima hajawasiliana na wewe?

Najua unaweza ukasema.."Ahhhh! sihitaji yote hayo" Mimi hapa nakwambia unayahitaji sana hayo mambo niliyoeleza hapo juu kutoka kwa mwanaume unayetaka kuwa na future nae.

Na unafahamu fika kwamba unayahitaji. Mwanaume sahihi kwako hataona taabu kuyafanya hayo na zaidi kwako akiamini anakutengeneza kuwa malkia katika paradiso yake,anajua utakuwa mbadala na msaada kwake na mama bora wa watoto wake!

Huu ni muda wa kujiongezea thamani.
Hebu acha tabia ya kuwasifia wanaume wa kawaida kwa sababu ya vijizawadi vya kupita na kuwaacha wale wenye kubeba ndoto na ubaadae wako kisa tu hawana pesa za kukupa vitu bora na vya thamani kwa sasa, angalia ng'ambo ya mto unakotaka kuvuka usiangalie hapo ufukweni uliposimama (mediocre men) !!!

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments