Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop, Aliyeshinda Medali ya Shaba Mara Mbili Amekutwa Amefariki Nyumbani Kwake


Mwanariadha wa Kenya  Agnes Tirop, aliyeshinda medali ya shaba mara mbili kwenye Mashindano ya Dunia amekutwa amefariki nyumbani kwake huko nchini Kenya.


Mwenyekiti wa Riadha nchini Kenya katika jiji la Nairobi, Barnaba Korir, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.


Ripoti zinaeleza kuwa alipatikana ndani ya nyumba yake akiwa na majeraha ya kuchomwa tumboni na taarifa kutoka Athletics Kenya ilieleza kuwa; ‘Tirop alipatikana amekufa nyumbani kwao huko Iten baada ya kudaiwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mumewe, bado tunajitahidi kupata maelezo zaidi kuhusu kifo chake,”.


Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda medali za shaba kwenye Mashindano ya Dunia ya 2017 na 2019 katika mbio za mita 10,000 na aliiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020 yaliyofanyika 2021 huko Tokyo, Japan.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments