Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ndege Mbili Kupokelewa Kesho Z’bar
NDEGE mpya 2 aina ya Airbus A220-300, zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania zimeondoka nchini Canada kuja Tanzania.

 

Ndege hizo zitapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume Mjini Unguja, Zanzibar kesho Oktoba 8, 2021 majira ya saa 9:00 Alasiri na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

 

Ndege hizi ambazo zimepewa majina ya Zanzibar na Tanzanite zitakamilisha hesabu ya ndege 11 zilizonunuliwa na kuwasili hapa nchini.

 

Kutoka Canada ndege hizi zinaendeshwa na Marubani wetu Capt Budodi na Capt Suad wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi.

 

Ndege nyingine 5 (Boeing 787-8 Dreamliner {2}, Airbus A220-300 {2} na Bombardier Dash 8 Q400 {1}) zimeshalipiwa na zitakuja baadaye.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments