Ticker

6/recent/ticker-posts

Nisha Bebe Afunguka Kuhusu SIRI ya Kufanikiwa Kwake na Kujenga Mjengo wa MaanaNimepokea simu na msgs nyingi watu kuomba ushauri jinsi ya kufanikiwa.

Naomba niwajibu hapa kiujumla.

Wapenzi kwanza mimi bado sijafanikiwa,sijafika nnapopataka ingawa kwa nilipo nnamshukuru Mungu mno.

Pili hakuna safari ya mafanikio ya siku moja,ni lazima upitie changamoto nyingi ili ndoto zako ziweze kutimia.

Nnaweza sema kitu fulani nimefanya kwa miaka mitatu.

Ila nilipigana,nilisaka,nilianguka na kuinuka kwa kuipigania kwa miaka zaidi ya 8.

Kwenye safari yangu nilichojifunza ni kuwa 1)mwingi wa shukurani,pale ninapopata na pale ninapokosa.

2)Uvumilivu na heshima ni silaha kubwa mno.

3)Kujishusha ndio siri kuu ya mafanikio.

4)kumuomba Mungu. Hakuna mafanikio yeyote pasipo nguvu zake.

5)kufanya kazi kwa bidii na kutokukata tamaa,hii iwe sehemu ya maisha yako.

6)penda unachofanya,jiongeze,buni mbinu mpya za kujiongezea kipato n.k

7)UPENDO usiwe na chuki,mwenzio akifanikiwa penda,penda wanaokuzunguka,penda unayemjua na usiyemjua,kuwa na moyo safi na thabiti.

8)WIVU kuwa na wivu wa maendeleo.

9.) SIRI kuwa msiri wa mambo yako ila usiwe mchoyo,usiseme jambo hadi liwe.

10.)MARAFIKI chagua marafiki wema kwani STANDARDS BASE WITH PEOPLE YOU FOLLOW

11)USIWE NA TAMAA ridhika na unachopata ila usibweteke.

Nnafurahi mnaponambia nawamotivate #kaziiendelee

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments