Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rosa Ree "Wanaume Msiogope Kuwa na Vitambi"

RAPA wa kike Bongo, Rosary Robert Iwole almaarufu Rosa Ree anasema kuwa, wanaume wasiogope kuwa na vitambi kwa kuhofia kuachwa na wake zao, badala yake wajikite zaidi kwenye kutafuta mkwanja tu; hapo kila kitu kitakwenda sawa, sawia.

Akipiga stori mbili-tatu na Gazeti la IJUMAA hivi karibuni, rapa huyo namba moja Bongo anasema kuwa, anashangaa kuona kuna wanaume bado wanahangaika kupunguza miili yao hasa vitambi, halafu wanasahau kutafuta pesa, mwisho wake ndiyo wanakuja kuitwa ‘vibenteni’, jambo ambalo siyo zuri.

P1Hivi karibuni niliposti video nikimshika mchumba wangu kitambi, nilitaka kuwaonesha watu kuwa kitambi siyo shida zangu na hasa wanaume ambao wanahangaika sana kutafuta six-packs (mbavu sita), halafu wanasahau kutafuta pesa mwisho wake ndiyo wanaanza kuitwa vibenten, kwa hiyo kaka zangu, amkeni tafuteni pesa mwanamke atakupenda tu jinsi ulivyo,” anasema Rosa Ree ambaye amechumbiwa hivi karibuni na jamaa aitwaye Petrousse.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments