Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rosa Ree rapa pekee Tanzania aliyetajwa tuzo za AFRIMMA
Kama tunavyofahamu kila mwaka tuzo mbalimbali hutolewa barani Afrika na pia duniani kote kupitia mkampuni na majarida tofautofauti mfano, AFRIMMA, AFRIMA, SOUNDCITY, MTV, MTV BAS BET  na nyinginezo nyingi.Siku ya jana zilitangazwa rasmi tuzo za AFRIMMA 2021 ambapo vimetolewa Kipengele vingi sana na miongoni mwa vipengele ambavyo watu walikuw awakivisubiria sana na vile ambavyo wataonekana au watawekwa wasanii kutoka Tanzania.

Miongoni mwa wasanii waliopo kwenye baadhi ya vipengele katika tuzo hizi kutoka Tanzania ni Alikiba, Diamond Platnumz, Nandy, Zuchu, Rosa Ree, pia maproducer na madirector kutpoka Tanzania mfano, Director Kenny, Producers S2kizzy na Kimambo.

Katika kipengele cha rapa bora wa kike Rosa Ree ameiwakilisha Tanzania ingawa hakuna rapa mwigine hata wa kiume aliyetajwa katika tuzo za AFRIMMA 2021.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments