RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Sabaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai akisoma maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi, Adam Kasekwa amesema mtuhumiwa huyo alisema Freeman Mbowe alipanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.
Katika ushahidi alioutoa leo, Oktoba 26, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kingai amesoma maelezo ya mtuhumiwa huyo kwamba Mbowe alisema Sabaya anahatarisha nafasi yake ya kuendelea kuwa mbunge wa Hai.

Ifuatayo ni sehemu ya maelezo ya mshtakiwa Adamu kama yalivyosomwa na RPC Kingai:

“Mbowe alituelekeza tufuatilie nyendo zake na tumdhuru kwa spray ya sumu. Ling'wenya alifuatilia mtu wa kupata sumu. Tarehe 27 tulirudi Dar na magari mawili pamoja na Mbowe na mlinzi wake.

“Baada ya kufika Dar tulifikishwa Mikocheni mimi na Ling'wenya tulipewa Sh200,000 tujiandae.Baadaye tulipewa nauli turudi Moshi. Agosti Mosi saa 11 alfajiri Mbowe alituita akasema tutekeleze maelekezo ya kumdhuru Sabaya.

“Akituonesha picha ya Sabaya na maeneo anauyopenda kutembelea. Alituelekeza baada ya kazi ya Sabaya turudi Dar kutekeleza kazi nyingine nyeti kulipua vituo vya mafuta na kushinikiza maandamano ili Serikaki ionekane imeshindwa maana inatuchukia sisi wapinzani.

“Yeye aliondoka kurudi Dar sisi tukabaki kutekeleza kumdhuru Sabaya Tarehe 3 Atosti tulienda eneo la Rao Madukani kwa dada yake Ling'wenya ili kubana matumizi maana Mheshimiwa alituachia Sh150,000

“Tulikamatwa na askari tukituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya na kupanga njama za ugaidi. Tuhuma hizo ni za kweli na pia kukutwa na silaha ni za kweli na nilikutwa na simu yangu ya Itel.

“Nilisaini hati ya kuchukuliwa mali na askari nao wakasaini. Nikachukuliwa kwenda Central Moshi. Uthibitisho haya maelezo ni ya kweli kwa saini.

“Muda wa kumaliza kuandika maelezo hayo ilkiuwa ni saa 3" 

Wakili wa Serikali Mwandamizi SSA Kidando alimtaka  ACP Kingai aelezee alichoelezwa na mshtakiwa huyo wa pili Adamu.

ACP Kingai :Alikiri kukutana na wenzake kwa ajili kwenda kwa Mbowe, alikiri kupewa nauli kwenda Moshi kukutana na Mbowe, alikiri kuwepo Moshi tarehe 24 -26 Julai 2020, alikiri kuwepo yeye na wenzake wawili akiwemo Ling'wenya na mtu mwingine.

“Alikiri tarehe 25 usiku kufanya mkutano yeye na Ling'wenya, Moses Lujenje maarufu Kakobe, Hassan Bwire na Freeman Mbowe"

SSA Kidando: Nini kiliendelea?

ACP Kingai : Alikiri kwenye mkutano alielekezwa na Mbowe kumdhuru DC Sabaya kwa njia yoyote ile.

SSA Kidando: Kitu gani kingine alikueleza?

ACP Kingai:  Shahidi pia alikiri kupewa pesa na Mbowe Sh150,000 kukidhi mahitaji hapo Moshi, alikiri Agosti Mosi 2020 alfajiri Mbowe aliwaita tena na kuwapa maelekezo, kwamba wahakikishe wanayafanyia kazi.

“Kumdhuru Sabaya na ili wawe na uhakika Mbowe aliwaonyesha picha ya Sabaya kupitia simu yake, aliwalekeza wamalize kazi hiyo ya Moshi halafu warudi Dar kufanya kazi nyingine nyeti.

“Alitaja kazi hiyo kwamba walipanga wakalipue vituo vya mafuta, lakini pia kufanya vurugu kwenye masoko na maeno ya watu wengi”.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kule kwa Sabaya kulionekana kutamu sana ghafla upandee huu umeharibu togwa

    ReplyDelete

Top Post Ad