Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Samatta ang’ara tena EUROPA league, Atupia
Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameifungia bao klabu yake ya sasa ya Royal Antwerp kwenye sare 2-2 dhidi ya Fenerbhance usiku wa jana kwenye michuano ya Ligi ya Europa.
Samatta alifunga bao hilo dakika ya pili ya mchezo na kuwapa uongozi Antwerp dhidi ya timu yake ya msimu uliopita lakini waliambulia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 ana kusalia mkiani mwa kundi D wakiwa na alama 1.

Bao hilo ni la pili kwa Samatta kwenye michezo mitatu ya michuano ya Europa Ligi tokea ajiunge na Antwerp mwezi uliopita hivyo kumfanya Mtanzania huyo kung;aa na kuendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania.

Kundi D linaongozwa na kinara, Eintranch Frankfurt ya Ujeruma ikiwa na alama 7, Olympiacos yapili ikiwa na alama 6, Fenerbhance yatatu ikiwa na alama 2 na Royal Antwerp ya Samatta ikishika mkia ikiwa na alama 1.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments