Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Rais Samia Awaonya Wanaotaka Kujua Rangi Yake Halisi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaonya viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia Mawaziri hadi Wakurugenzi kutumia vizuri fedha za mkopo jumla ya Shilingi Trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).


Onyo hilo amelitoa jana Jumapili Oktoba 10, 2021 wakati akihutubia taifa kupitia uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

 

”Kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi, mkinitazama hivi mnasema Mhe. Rais ni mweupe lakini nina rangi halisi, kwa hiyo wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi wajaribu kudokoa pesa hizi au wabadilishe matumizi ya fedha hizi bila maelewano,”amesema Rais Samia

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments