Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Shabiki wa City apata Coma kwa kupigwa na kitu kizito, mashabiki wa Club Brugge wahusishwa
Shabiki wa Man City apigwa na kitu kizito na kupata Coma, mashabiki wa watano wa Club Brugge mbaroni, City ikiwanyoosha 5-1 Champions League.Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Ubelgiji baada ya shabiki mmoja wa Manchester City kushambuliwa mpaka kupata Coma na wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa Club Brugge usiku wa kuamkia leo baada ya mchezo wa Champions League ambapo City iliondoka na ushindi mnono wa 5-1.Mtu huyo mwenye umri wa miaka 63, raia wa Ubelgiji alikuwa ni miongoni mwa mashabiki wa City kutoka kundi linalojiita ‘Blue Moon Belgium,” ambaye alishambuliwa wakati akirejea nyumbani akitoka kuangalia mchezo huo ambapo timu yake aipendayo ikiondoka na ushindi huo mnono.

Polisi wameripoti kuwa kulikuwa na makabiliano kutoka katika sehemu ya kuegesha magari na ndipo akashuhudiwa mtu huyo akiwa katika hali mbaya hadi kukaribia kufa.

Shabiki huyo aliyefahamika kwa jina moja la Guido, alikutwa akiwa amevalia skafu ya Manchester City shingoni kwake alipigwa na kitu kizito kichwani hayo ni kwa mujibu wa mtoto wake, Jurgen.

Guido aliwahishwa Hispitali ya AZ Maria Middelares akiwa hajitambui kwa mujibu wa gazeti la Ubegiji la Het Laatste Nieuws.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments