Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Spika Ndugai apangua kamati za Bunge, Polepole ahamishwa
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko madogo ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, ambapo amemhamisha Mbunge Humphrey Polepole kutoka Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenda Kamati ya Sheria Ndogo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 na Spika wa Bunge, Job Ndugai imeeleza kuwa mabadiliko hayo madogo ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge yamefanyika kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 135 (3) – (5) ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la Juni 2020.

Aidha, Spika Ndugai amemhamisha Godwin Kunambi kutoka kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenda Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii.


 
Spika amewateua baadhi ya wabunge katika kamati kadhaa ambapo Asia Halamga na Agnes Marwa wamepelekwa Kamati ya Masuala ya Ukimwi.

Spika Ndugai amemteua Dk Faustine Ndugulile kuwa mjumbe wa kamati ya sheria ndogo na kamati ya masuala ya Ukimwi.

Dk Medard Kalemani na Dk Leonard Chamuriho wameteuliwa kuwa wajumbe wa kamati ya sheria ndogo.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments