Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Tiwa Savage Afunguka Kuhusu Mtu Anayetaka Kuvujisha Video yake ya Ngono


Nyota Tiwasavage kutoka Nigeria kwenye mahojiano yake leo na kituo cha Power 105.1, nchini Marekani, akizungumza kwenye show ya 'The Angie Martinez Show' amefunguka kuwa jana ametumiwa video yake akiwa FARAGHA (mkanda wa ngono) na mpenzi wake.

Tiwa ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake binafsi, amekiri kwamba, video hiyo inaonyesha kuwa ni yake kwani anaonekana akiwa na mpenzi wake aliyenaye sasa.

"Jana wakati nikiwa njiani ndani ya gari langu, meneja wangu alinitumia ujumbe kwa njia ya sms kwamba kuna video amenitumia niitazame. Nilishtuka nilipoitazama na kujiuliza kuwa ameitoa wapi, ilikuwa kama dakika 20 kufanyika kwa tukio hilo.

"Meneja alinieleza video hiyo ya FARAGHA alitumiwa na kijana tuliyenaye kwenye timu yetu" - aliendelea Tiwasavage, "Nilichanganyikiwa na kumuuliza meneja wangu kuwa tunafanyaje?

"Meneja akaniuliza ni kiasi gani anahitahiji tumpatie? Nikamjibu hapana, kwa sababu tukimpa pesa leo, atarudi tena baada ya miezi 2 mbele atahitaji tena pesa, kwahiyo siwezi ruhusu mtu kuniibia kwa kitu ambacho sio halali" - alimalizia Tiwasavage akizungumza na mtangazaji Angie Martinez.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments