Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Tutatumia kila mbinu wananchi wapate chanjo ya UVIKO - 19 Singida - RC Mahenge
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amesema watatumia kila mbinu ili kuona wananchi wa mkoa huo wanapata chanjo ya Uviko-19.
Dkt.Mahenge ameyasema hayo leo kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya jamii  (PHC) Mkoa wa Singida kilicho keti kuhusu utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19.“Tumekwisha anza kuona matokeo mazuri ya watu kujitokeza kupata chanjo, hii inatokana na kazi nzuri na mbinu mbalimbali za uhamasishaji naomba tusimame hapo na twende tukaeneze hizo juhudi ninachohitaji ni kuona watanzania wengi wanapata chanjo,”. alisema Mahenge.
Alisema zitatumika kila mbinu katika kukamilisha kazi hiyo kwani kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani hivyo ni wajibu wetu tufanye kila liwezekanalo ili wabaki mamba na kuachana na hao kenge ambao wanazohofisha jitihada hizo.

Alisema kazi hiyo inawezekana hasa baada ya hizi siku chache kuongezeka kwa idadi ya wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema muitikio wa wananchi kupata chanjo hiyo ni mkubwa zaidi maeneo ya vijiji tofauti na mijini ambapo alitolea mfano wa Singida Mjini ambayo imepitwa na Singida Vijijini hivyo akaomba uhamasishaji katika maeneo ya mijini uongezewe nguvu.


Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Joseph Kyense aliiomba Serikali iendelee kuleta chanjo nyingi zaidi ili kila mwananchi aweze kuchagua chanzo atakayoipenda badala ya kuwa na moja tu.


Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili alisema kupitia mpango huo Shirikishi na Harakishi wananchi wamekuwa na muitikio hasa baada ya kueleweshwa umuhimu wa chanjo hiyo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Sema na Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu alisema kesho kwa kushirikiana na Civil Society Foundation watakuwa na kikao na Mashirika 50 ya mkoani hapa kwa ajili ya kuona mchango wao wa uhamasishaji wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.
Mwenyekiti wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida Sheikh Hamisi Kisuke alisema zoezi la kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba ili watu wajitokeze kupata chanjo  limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza idadi ya watu tofauti na mwanzo.


 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments