Ticker

6/recent/ticker-posts

Twaha Kiduku Ampa Pole Dulla Mbabe "Hata Kina Tyson Walishawahi Kupigwa"


Bondia kutoka mji kasoro bahari Morogoro @twaha_kiduku ametoa pole kwa bondia mwenzake mtanzania @official_dullahmbabe kwa kupokea kipigo na kupoteza pambano lake dhidi ya Bondia mkongo Tshimanga Katompa aliyeibuka mshindi kwa pointi kwenye pambano la raundi 10 usiku wa kuamkia leo hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram bondia Twaha kiduku ambae anatajwa kama hasimu wa bondia huyo ambae wamewahi kuzichapa mara kadhaa, ameandika;↓

“Pole sana Brother uwezi kua champion bila kupoteza ata wakina Taison walipoteza na wakajifunza ndioman wakafanya makubwa usikate tamaa bado nafasi unayo na uwezo pia unao mchezo unamatokeo 3 kushinda,kudrow na kupoteza usivunyike moyo kuanza upya sio ujinga mfano ww ulinipiga round ya 1 nikaanguka lakini sikukata tamaa pambana Brother ndio mchezo ulivyo”.Hili ni pambano la pili mfululizo kwa bondia huyo maarufu kutoka mkoa wa pwani kupoteza katika siku za hivi karibuni.

✍🏾@keviiiy.iam


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments