Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wapinzani wa Simba CAF Waingiwa Mchecheto

KOCHA Mkuu wa Jwaneng Galaxy, Morena Ramoreboli, amesema wanatakiwa kufanya kazi nzito ili kuhakikisha wanaiondoa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwani wapinzani wao hao wana kikosi bora.

 

Simba katika michuano hiyo, wanaanzia ugenini kwenye hatua ya kwanza kwa kucheza dhidi ya Jwaneng ya Botswana. Mechi ya kwanza ikichezwa Oktoba 17, kisha marudiano Oktoba 22.

 

Morena alisema: “Ninaheshimu sana uwezo wa Simba ambao wameuonesha katika miaka ya hivi karibuni, katika michuano ya kimataifa wamefika hatua nzuri, ni timu kubwa, hivyo tunatakiwa kupambana haswa ili kutimiza malengo yetu ambayo ni kusonga mbele.

 

“Tunayo faida ya kuanzia nyumbani, hivyo tunatakiwa kufanya vizuri katika mchezo wetu wa mwanzo, tutapambana kuhakikisha tunasonga mbele, hakuna namna nyingine zaidi ya kwenda kupambana na Simba.”

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments