Watanzania Milioni Saba Wana Matatizo yanayohusiana na Afya ya Akili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Wakati Dunia ikiadhimisha Siku ya Afya ya Akili kesho Jumapili Oktoba 10,2021, imeelezwa kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni saba wenye matatizo yanayohusiana na afya ya akili.


Hata hivyo, sababu mbalimbali zimetajwa kusababisha matatizo ya afya ya akili huku Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa na idadi kubwa ya wenye matatizo hayo.



Miongozi mwa sababu zilizotajwa kuchochea tatizo hilo ni msongo wa mawazo, ugumu wa maisha na matamanio ya kuwa na maisha bora.



Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa magonjwa yasiyoambukiza, Dk Shedrack Makubi amesema sababu ya Dar es Salaam kuwa na wagonjwa wengi ni kutokana na wingi wa watu katika jiji hilo ambalo lina mkusanyiko kutoka mikoa mbalimbali.



Pia, mazingira na harakati za kutafuta maisha kwa wakazi wa jiji hilo, zimetajwa kuwa kichocheo cha watu wengi kujikuta kwenye matatizo hayo ya kiafya.



Dk Makubi alitaja sababu nyingine ni matumaini ya watu mbalimbali kuwa Dar es Salaam kuna fursa nyingi za maisha na ajira hivyo, wanakuja kwa ajili ya kutafuta lakini, wanapofika mambo huwa tofauti na matarajio.



Alisema kuwa mambo yanapokuwa tofauti na matarajio, baadhi hujikuta kwenye wakati mgumu na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa likiwemo matumizi ya dawa za kulevya.



Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kufikia mwaka 2020 watu bilioni moja walikuwa wanaishi na magonjwa ya akili huku wengi walio katika hatari ni wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 39.



Mkurugenzi wa Hospitali ya Magonjwa ya afya ya akili ya Mirembe, Dk Paul Lawala alisema ugonjwa wa afya ya akili ni tatizo kubwa duniani kwani takwimu zinaonyesha watu milioni 300 duniani wanakabiliwa na tatizo la afya ya akili, ambapo wanahitaji msaada wa kisaikolojia na waliofikia viwango vya juu wanahitaji matibabu.



Undani magonjwa ya akili

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dk Omary Ubuguyu, amesema kuna magonjwa zaidi ya 340 ya akili yaliyogawanywa katika makundi tofauti.



“Kwa kiasi kikubwa magonjwa ya akili yanahusishwa na kupotea kwa nguvukazi, kwa kuwa magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati, wagonjwa wengi hushindwa kurudi kwenye uwezo wao na hivyo, kuathiri uwezo wa uzalishaji.

&t;br />

Kwa jumla magonjwa ya akili yanachangia kwa zaidi ya asilimia 40 ya athari za kiafya kwa mtu mmoja mmoja na jamii,’’ amesema.



“Hii inamaanisha kuwa, jamii yetu inapaswa kuwekeza kwenye afya ya akili kwa kiasi kikubwa zaidi. Uwekezaji katika afya ya akili haulengi tu katika kutibu wale wenye mahitaji, lakini unalenga katika kuimarisha afya ikiwamo udhibiti kwenye matumizi ya vilevi kama pombe na sigara, kufanya mazoezi, lishe bora na kuimarisha uhusiano kwenye jamii,” amesema Dk Ubuguyu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HELLO GET OUT OF FINANCIAL MESS WITH THE HELP OF drbenjaminfinance@gmail.com

    I have been in financial mess for the past months, I’m a single mum with kids to look after. My name is REBECCA MICHAELSON, and am from Ridley Park, Pennsylvania. A couple of weeks ago My friend visited me and along our discussion she told me about DR BENJAMIN OWEN FINANCE of drbenjaminfinance@gmail.com that he can help me out of my financial situation, I never believed cause I have spend so much money on different loan lenders who did nothing other than running away with my money. She advised, I gave it a try because she and some of her colleagues were rescued too by this Godsent lender with loans to revive their dying businesses and paying off bills. so I mailed him and explain all about my financial situation and therefore took me through the loan process which was very brief and easy. After that my loan application worth $278,000.00USD was granted, all i did was to follow the processing and be cooperative and today I am a proud business owner sharing the testimony of God-sent Lender. You can as well reach him through the Company Email drbenjaminfinance@gmail.com

    THANK YOU VERY MUCH

    ReplyDelete

Top Post Ad