Ticker

6/recent/ticker-posts

Watu 7 wa familia moja wanusurika kifo Kirumba jijini Mwanza.
Watu 7 wa familia moja katika mtaa wa Magomeni Kirumba Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika.
.
Moto huo ulizuka leo asubuhi, kwenye nyumba ya Bi.Anna Ng'habi iliyopo jirani na Kituo Kikuu cha Polisi Kirumba umbali wa Mita 40, kabla ya gari la jeshi la zimamoto na uokoaji kufika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto.
.
Wakati Askari wa Zimamoto wakipambana kuzima moto huo, hali ilizidi kuwa tete, baada ya nyaya za umeme ambao ulikuwa bado haujakatwa na mafundi wa shirika la umeme nchini, kuanza kutoa cheche za moto na kusababisha watu waliofurika eneo hilo kuanza kutimua mbio ili kujiokoa.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments