Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Watu Binafsi Waliofunga ving'ora Kwenye Magari yao Kushtakiwa


Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limesema litafanya msako wa kuyabaini magari binafsi yaliyofungwa ving’ora bila kufuata utaratibu na wafungulia mashtaka wamiliki wa magari hayo kwa kuvunja sheria ya usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi ameyasema hayo wakati akizindua wiki ya usalama barabarani na kueleza kuwa hatosita kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa magari binafsi watakaobainika kufunga ving’ora kwenye magari yao kinyume na sheria.
 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments