Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wema Ahurumiwa, Atiwa Moyo

BAADA ya Vanessa Mdee na mpenzi wake, Rotimi kutanganaza kwamba wamebarikiwa mtoto wa kiume na watu mbalimbali kupongeza, Wema Sepetu alisema kuwa ana wivu, lakini licha ya hayo yote alimpongeza Vanessa.

 

“Im sooo jealous. Congrats my baby,” Wema alimwandikia Vanessa.

Kwa upande wake Vanessa alimshauri na kumwambia kwamba wakati wake utafika.

 

Hata hivyo, kufuatia majibizano hayo kati ya Wema na Vanessa wanamitandao wamemuhurumia na kumtia moyo Wema huku wakisema siku moja Mungu atamshangaza na atakuwa na ushuuda wake.

 

Mapema mwaka huu, Wema alisema kwamba licha ya kutarajia mengi kutoka kwa mmoja wa wapenzi wake, lakini waliachana kwa sababu hakuwa na uwezo wa kumpa mtoto.

 

“Kwa kweli nilikuwa nikitarajia kuolewa naye, lakini jambo moja au tuseme moja ya sababu ambazo zilisababisha kuachana kwetu ni kutokuwa na uwezo wa kumpa watoto.

 

“Ilikuwa mbaya kwangu kwa sababu kama mwanadamu, nilikuwa na matarajio yangu na nilikuwa nikitarajia mapenzi yetu yangechipuka na kuimarishwa na mtoto,” alisema Wema.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments