Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wenger: Salah Ndiye Bora Duniani

KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah
ndiye bora duniani kwa sasa.

 

Wenger amesema Mmisri huyo amekuwa akifunga mabao ambayo hakuna anayetarajia kuwa anaweza kufunga.
Salah amekuwa moto msimu huu akiwa amefunga mabao kadhaa muhimu na alifunga mawili kwenye ushindi
wa mabao 3-2 dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, juzi.


Wenger amesema kuwa mchezaji huyo ni mbunifu, mtengenezaji na mtu ambaye anaweza kufunga mabao kwenye engo yoyote ile.


Salah amekuwa akiweka rekodi kila mara na juzi aliweka rekodi ya kufunga kwenye michezo tisa mfululizo.
“Salah ni mchezaji mkubwa sana, nafikiri kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa kuwa naona anaweza kufunga mabao ambayo mchezaji mwingine hawezi kufunga.


“Maisha yake ya nyuma yanamfanya afanye jambo lolote, aliwahi kucheza soka mtaani na hicho ndiyo kinamfanya aweze kupiga chenga wachezaji watatu wanne kwa pamoja. Ni mjanja na mwenye uwezo mkubwa sana,” alisema Wenger.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments