Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Wolper Aibuka Bila Rich Mitindo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

MWANAMAMA mkali wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper au Mama P ameibua gumzo baada ya kuibuka kwenye pati kwa mara ya kwanza bila baby daddy wake, Rich Mitindo.

 

Wolper aliibuka mwenyewe kwenye pati ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel iliyofanyika nyumbani kwa staa huyo, Tegeta jijini Dar, usiku wa kuamkia jana, Alhamisi.

Kitendo hicho kinatafsiriwa kwamba ni ishara mbaya kwamba, huwenda bundi ametua kwenye paradisho ya wawili hao.

“Mh yule siyo Wolper? Mbona leo jeshi la mtu mmoja? Au tayari bundi ametua penzi lao? Kiukweli tumezoea kuwaona pamoja hivyo hatuamini tunachokiona,” alisikika mmoja wahudhuriaji kwenye pati hiyo.

Hata hivyo, katika utetezi wake, Wolper alilieleza Gazeti la IJUMAA kuwa, Rich Mitindo alimtumia usafiri wa kumpeleka kwenye shughuli hiyo akimuomba kuwa, atachelewa hivyo atangulie na atamfuata baadaye.

Wolper na Rich Mitindo ni wachumba ambao mwaka huu wamejaaliwa mtoto mmoja aitwaye Pascali au P.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments