Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Yanga Walifukuza Timu Nzima Mpaka Baba Yangu

UONGOZI wa klabu ya Yanga, kupitia kwa ofisa muhamasishaji wake, Haji Manara, leo Oktoba 26, wamewasihi mashabiki na wapenzi wa Yanga kujitokeza katika
11 mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Azam FC itakayopigwa Jumamosi hii katika DImba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari katika Hoteli ya Serena, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema dhamira ya Yanga mwaka huu ni kuchukua ubingwa wa Ligi.

“Tunataka taji letu la mara 28. Azam ni timu nzuri tunawaheshimu, ndio wapinzani wetu msimu huu na si0l0} P} wengine huko. Yanga ni kitu kingine ndugu yangu msikie hivyo hivyo.

“Mimi nilikuwa maarufu sehemu nyingine ila kuja Yanga umaarufu wangu umeongezeka mara milioni. Yanga ni timu iliyoanzishwa na viongozi wakubwa wa nchi hii, achana na timu iliyoanzishwa na watu wamekaa wakicheza bao.


 
“Viongozi wa Yanga hawajioni miungu watu wanakubali nadharia za kimpira, hawakubali nadharia za kusalitiana. Yanga waliwahi kufukuza timu nzima na baba yangu akiwemo, kina Tenga na Director General mzee Tabu Mangala.

“Sisi tulikuwa tunalaumiwa pre-season yetu haikuwa nzuri sawa tumekubali ila nyie mlioimarika tulipokutana ilikuwaje?

“Timu kubwa mkifungwa mnaanza kusingizia kusalitiana? Hata tumlete Messi acheze na kina Mayele na mbele yao au nyuma yao yupo Ronaldo lazima tutafungwa na huo ndio mpira. Wewe huna Messi, huna Ronaldo timu yako isifungwe kwanini?


“Naomba niwaambie wana Yanga wenzangu, pamoja na ubora wa Kikosi chetu hatakama tumlete Messi kwenye timu yetu lakini ipo siku tutafungwa, hivyo ndivyo mpira ulivyo. Tusiwe Kama wenzetu wakifungwa wanasema wamesalitiana,” amesema Manara.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments