Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Young Lunya "Tunafanya Ngoma Mbili na Diamond PlatnumzMsanii wa Hip Hop Bongo, Yong Lunya amesema yeye na mwimbaji wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz wamepanga kurekodi nyimbo mbili pamoja ambazo kila mmoja atakuwa na yake.

Kauli ya Lunya inakuja mara baada ya wawili hao kukutana Afrika Kusini ambapo wote walienda kwa ajili ya maandalizi ya albamu zao na ikasemekana huwenda walirekodi ngoma.

Young Lunya amesema muda wowote watarekodi.

"Bado hatujarekodi, mimi na Diamond tumepanga kufanya muda mrefu sana lakini nafikiri tu yupo bize lakini ni kitu ambacho kipo kabisa, tulishapanga tutafanya madude moja la kwake moja la kwangu, kwa hiyo nipo kwenye mchakato," amesema Young Lunya.

Lunya atakuwa Rapa mwingine wa kizazi kipya kufanya kazi na Diamond mara baada ya Young Killer ambaye alishirikishwa kwenye wimbo uitwao Pamela ambao unapatikana kwenye albamu yake, A Boy From Tandale iliyotoka Machi 2018.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments