Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Aliyetumikia Kifungo Miaka 42 Gerezani Kimakosa Aachiwa

MMAREKANI mwenye asili ya Afrika, Kevin Strickland mwenye umri wa miaka 62 ameachiliwa huru mara baada ya kutumikia kifungo cha miaka 42 gerezani kimakosa.

Strickland alikamatwa mwaka 1978 na kufunguliwa mashtaka ya mauaji, na mnamo Juni 1979 Strickland akiwa na umri wa miaka 18 alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na kukutwa na hatia ya mauaji ya watu watatu huko Kansas City, Missouri nchini Marekani, ambayo yeye mwenyewe alikana kutohusika na mauaji hayo.

Hivi karibuni mwendesha mashtaka Jean Peters Baker, alituma maombi katika mahakama ya Missouri iliyotoa hukumu ya kifungo kwa Strickland kurudia na kupitia tena ushahidi uliotumika awali, ambapo baada ya hapo ilithibitika kuwa hakukuwa vithibitisho kamili vya mauaji hayo na hivyo Jaji huyo aliamuru Strickland aachiwe huru.

Strickland aliachiwa huru juzi, Novemba 23, 2021 na baada ya kuachiwa alisema maneno haya “sikufikiria siku hii ingefika.”

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments