Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Amuua Mwanaye Akimlazimisha Aolewe kwa Mahari ya Ng'ombe 15
Binti wa miaka 17 wa kijiji cha Lufubu, wilayani Uvinza adaiwa kuawa na baba yake mzazi Kulwa Juakali (40), baada ya kukataa kuolewa kwa mahari ya ng'ombe 13.

Akizungumza leo, Novemba 12, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Novemba 10 mwaka huu, ambapo baba huyo akishirikiana na ndugu zake wawili walimpiga binti huyo kwa fimbo na kumsababishia jeraha sehemu ya kichwani ambalo limesababisha kifo chake.

Kamanda Manyama amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu ambao ni baba, baba mkubwa (Shija Juakali-(44) na baba mdogo Majiba Juakali-(29) kwa upelelezi zaidi.

"Upelelezi wa shauri hili unaendelea watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria mara baada ya taratibu za upelelezi kukamilika," amesema Kamanda Manyama.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments