Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Baraka The Prince "Gigy Money si Lolote Alikuwa Chawa wa Video Vixen Wangu Kabla Hajatoka"
Ishu ya Shilole na Alikiba ilipelekea kutokee mgogoro pia kati ya Gigy Money na Barakah The Prince, huku Gigy Money akijiapiza kutoa mafile ya Barakah. Hasa kwanini Baraka ameamua kukausha wakati si kawaida yake?

Kwenye Empire ya EFM, Barakah amedai hana tatizo na Gigy Money maana yeye amechangia kumuweka hapo alipo hivi sasa,yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo kabisa kumuweka kwenye video yake inayoitwa Siachani nawe, alimfahamu Gigy Money kama chawa wa Video Vixen wa Video yake hiyo iliyotoka June 18,2015. Lakini pia Kingine amedai Gigy ni mdogo wake na hawezi bishana na mtoto wa kike.


HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL APP, DOWNLOAD HAPA UWE NAYO KWA SIMU YAKO..USIPITWE

Kingine Baraka ameeleza sababu za EP yake iliyokuwa ikitarajiwa itoke Mwezi March mwaka huu ila ikawa kimya hadi sasa, The Prince amedai ashawahi fanya EP hivyo akaona raundi hii aje kitofauti na si kufanya kama alivyowahi fanya mwanzo, na mwezi huu mashabiki zake wategemee makubwa maana anaachia package yake.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments