Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Breaking News : Maduka 43 Yateketea kwa Moto..Kunani Ajali za Moto Kila Kukicha?


MADUKA 43 yameteketea alfajiri ya leo Jumanne, Novemba 16, 2021 baada ya jengo moja ndani ya Soko la Manzese, wilayani Tunduma mkoani Songwe kuteketea kwa moto.


Maduka 33 yaliyoteketea yalikuwa na vifaa huku maduka 10 yakiwa hayana kitu katika soko hilo ambalo lipo mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.


Kaimu Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Songwe amesema kuwa walipata taarifa za moto huo mnamo saa 11 alfajiri na kuwahi kufika katika eneo la tukio mpaka muda wa saa 3 asubuhi zoezi lililokuwa likiendelea ni kuudhibiti moto huo.

Hata hivyo hakuna madhara ambayo yameripotiwa kutokea kwa binadamu.

Kwa taarifa Zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments