Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Fahamu Dini Mpya inayozua Mjadala Mashariki ya kati
Katika maadhimisho ya miaka kumi ya nyumba ya familia ya Misri inayohusisha viongozi wa dini za Kiislamu na wenzao wa Kikristo , kampeni ya umoja wa kidini ilianza nchini humo , lakini Imamu mkuu wa Al -Azhar, Ahmed Al Tayyib , aliikosoa dini mpya ya Abrahamu inayodaiwa kuzua mjadala katika eneo la mashariki ya kati.


Ukosoaji wake kwa mara nyengine umesabisha kuangaziwa upya kwa dini hiyo ya Abrahamu , ambayo kwa kipindi cha mwaka mmoja imezua hisia kutoka kwa mataifa ya Kiarabu.Je dini ya Abrahamu ni ipi?

Kufikia sasa hakujakuwa na tangazo rasmi kuhusu uwepo wa dini hiyo. Hakuna hata mtu mmoja aliyehusika katika uanzilishi wake mbali na uwepo wa wafuasi wake.Si hayo pekee hakuna hata maadishi yake yaliopo. Katika hali hiyo , swali ambalo limekuwepo ni je dini hii ya Abrahamu ni ipi?Kwasasa inaweza kuonekana kama mradi unaohusishwa na dini.Chini ya mradi huu , katika siku za hivi karibuni , juhudi zimeanzishwa kuanzisha dini kupitia jina la mtume Abraham , wakiihusisha na vitu vinavyotekelezwa na dini hizi tatu za Uislamu, Ukristo na Judaism .Lengo lake ni kutegemea vitu sawa vinavyohusishwa na dini hizo tatu. Wakati huohuo , dini hiyo haihusishi masuala tata yanayotofautisha dini hizo tatu.Kwanini sasa?

Ukweli ni kwamba mazungumzo kuhusu dini hiyo yalianza mwaka mmoja uliopita na utata pia umeonekana kuihusu.Ijapokuwa watu wengi wanajaribu kuelewa kwanini Imamu huyo alizungumzia kuhusu suala hilo. Kwasababu kwasasa kuna watu wengi ambao wamesikia dini hiyo kwa mara ya kwanza kutoka kwa Al Tayyeb.Hotuba iliotolewa na Sheikh wa msikiti mkuu wa Al-Azhar inashirikisha mazungumzo ya kuishi kwa pamoja kati ya waumini wa dini tofauti.Uanzishi wa nyumba ya familia ya Misri ulifikiriwa baada ya mazungumzo kati ya Papa Shenouda 111 na ujumbe kutoka Al Azhar kufuatia mapinduzi ya mwaka 2011 mjini Alexandria, Misri.Ni sawa na pia ni matarajio ya wengi kuzungumzia kuhusu watu kuishi kwa pamoja kati ya dini mbili.Pia inasemekana kwamba Sheikh al-Azhar alifikiria kwamba ni sawa kuzungumzia kuhusu wanaopigania dini ya Abrahamu kutoka kwa nyumba ya familia hiyo.Al-Tayyab alianza kwa kusema, " Kwa hakika wanataka kuzungumzia mkanganyiko wa udugu baina ya dini mbili za Kiislamu na Kikristo na mashaka yanayojitokeza kuhusu kuchanganya na kuunganishwa kwa dini hizo mbili... ""Wale wanaotaka kuunganisha Ukristo, Uyahudi na Uislamu kuwa dini moja watakuja kusema kuhusu ukombozi kutoka kwa maovu yote," alisema.Kwanini Tayyab alishutumu?

Al-Tayyib alikana wito wa kujiunga na dini mpya ya Abrahamu . Alisema kwamba dini hiyo mpya inayozungumziwa haitakuwa na rangi, ladha ama hata harufu.Pia alisema kwamba wahubiri wanaounga mkono dini hiyo pia watasema kwamba watamaliza mizozo iliopo lakini ukweli utakuwa ni wito wa uhuru wa kuabudu kwa mapenzi yao.Al Tayyeb pia alisema kwamba wito wa kuleta dini tofauti pamoja ni ndoto inayoshangaza badala ya kuwaelewesha watu kuhusu ukweli na asilia. Kulingana na yeye ni vigumu kuwaleta pamoja watu wa dini tofauti.Al-Tayyib aliongezea kwamba "Ni kitu kimoja kuheshimu dini ya mwengine na ni suala tofauti kuikubali Imani hiyo.."Hotuba ya Al Tayyab kuhusu dini ya Abrahamu imesifiwa na wengi katika mitandao ya kijamii , akiwemo Abdulah Rushdie , ambaye alisema kwamba Al Tayyib aliliangamiza mapema wazo la dini hiyo, wakati wengine wakisema kuwa "hakuna pingamizi kwa wito huu wa kumaliza mabishano na migogoro."Madai ya kisiasa chini ya kivuli cha kutumia dini

Sheikh wa Al-Azhar hakutaja mwelekeo wowote wa kisiasa wa wito wa dini hiyo katika hotuba yake.Lakini wengine kwenye mitandao ya kijamii wamekataa mwaliko huo kama "wito wa kisiasa uliofunikwa kwa pazia ya kidini".Miongoni mwao ni kuhani wa kanisa la Coptic nchini Misri, mtawa Hegomen Niamey, ambaye alisema kuwa "dini ya Ibrahimu ni wito wa kisiasa chini ya kivuli cha udanganyifu na utumianaji mbaya."Miongoni mwa wanaoikataa dini hiyo mpya ni wale wanaoiona kuwa ni sahihi kiitikadi lakini wanaona kuwa ni kambi ya kisiasa tu yenye lengo la kuhalalisha na kuimarisha uhusiano na Israel hasa katika ulimwengu wa Kiarabu.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments