Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Fahyma ‘Atamuua’ Paula

MADAI kwamba, mwanamitindo Fahyma amerudiana na baba wa mtoto wake, Rayvann zinatajwa kuwa zitamuua mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Paula Kajala.

 

Tangu kuondoka kwa Paula kwenda masomoni nchini Uturuki na kumwacha Rayvanny Bongo, yamesemwa mengi; lakini kubwa ni yeye kurejesha majenzi kwa mzazi mwenzake, Fahyma.

 

Watu wa karibu wa familia ya Paula wanasema kuwa jambo hilo linampa wakati mgumu mno mrembo huyo kiasi cha kuhisiwa kutofanya vizuri kwenye masomo yake.

 

Tangu Paula ameondoka Bongo, Fahyma amecharuka na kuanza kufanya mambo ambayo yanaaminika ni ya kumvuta Rayvanny ili warejeane.

 

Mfano ni madai kwamba, hivi karibuni Fahyma na Rayvann walionekana pamoja kwenye mgahawa unaosemekana kumilikiwa na jamaa huyo.

 

Pia Fahyma amekuwa karibu mno na mashabiki wa Rayvanny ambapo amekuwa akiposti video akiimba nyimbo za Rayvanny huku akiposti picha zake za mitego ambazo wengi wanaamini ni kwa ajili ya kumtega jamaa huyo.

 

Mara nyingi amekuwa aki-tag jina la Rayvanny na kusema yeye ni mrembo kupita mrembo yeyote akimlenga Paula.

Hata hivyo, mashabiki wengi wa Fahyma wamekuwa na shauku ya kusikia amerudiana na Rayvanny, lakini jamaa huyo amekuwa akimpotezea kwa kila kitu anachomfanyia.

 

Kubwa zaidi ni Fahyma kuwa amekuwa akikiri waziwazi kwamba anampenda mno Rayvanny na amekuwa hana kigugumizi kwenye hilo. Fahyma amekuwa akiamini ipo siku moja atarudiana na Rayvanny au Baba Jaydany.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments