Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Gardner "Nasikia Mjukuu Wangu Baba ni Diamond Platnumz"
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Gardner G Habash ambaye ni baba mzazi wa msanii Malkia Karen amefunguka kuhusiana na mwanawe huyo. Pia Gardner amezungumza kuhusu baba wa mjukuu wake aliyezaliwa hivi karibuni na Malkia Karen.


“Kuhusu kusema nilikuwa nataka mwanangu apate mwanaume au mume mwenye uwezo, nilikuwa namaanisha nilikuwa na-wish; yaani matamanio na kila mzazi ana matamanio mazuri kwa mwanawe hivyo nilikuwa na matamanio ya mwanangu awe na mwanaume mwenye uwezo na yale ni matamanio kwa hiyo yanaweza kutimia au yasitimie,” anasema Gardner kuhusiana na kauli yake ya siku nyingi kwamba, alitaka Malkia Karen awe na mwanaume mwenye uwezo na kuendelea;“Kuhusu mwanangu kuzaa kabla hajaolewa, kwangu ni kitu cha kawaida maana hata yeye nilimzaa kipindi
niko chuo, nilipendana na mama yake tukapata mtoto mapema.


Nakumbuka kipindi anajifungua nilikuwa JKT (jeshini), nilivyopata taarifa nilijaribu kutoroka maana mtoto alikuwa Mabibo (Dar) nilikuwa natamani sana kumuona, lakini ilishindikana.“Kuhusu baba wa mtoto wake hata mimi nasikia kwenye mitandao ya kijamii kuwa mtoto ambaye ni mjukuu
wangu ni wa Diamond ila nasikiasikia tu na mimi na kusema niweke wazi baba wa watoto wa Karen siwezi maana hata yeye hayupo tayari kuliweka suala hilo wazi kwa sasa…”

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments