Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Haji Manara, Mwana SIMBA Anayeteswa na Mzimu wa Mo DewjiTangu Haji Manara amehamia Young Africans Sports Club ni kama ameshajua kuwa brand yake ime drop kiasi fulani. Hana ule mvuto tena kama aliyokuwa nao hapo awali.
Ushawishi wake kwenye jamii ya soka umeshuka tofauti na alivyokuwa Simba SC Tanzania kwa miaka yote.

Na hii ni kutokana kwamba amejitengenezea uadui kwa mashabiki mpira. Mashabiki wa Simba hawamtaki na hata kule Yanga napo kuna makundi mawili; wapo mashabiki wanaojilazimisha kumwelewa kwa sababu kaletwa na bosi wao (GSM), pia wapo wale wasiomukubali kwa sababu ya kejeli na matusi aliyokuwa akiwatolea pindi yupo Simba. Hivyo amepoteza mashabiki wote wa Simba na kule yanga amepata nusu. Kimsingi hapa kachemka kiasi fualni.

Hili jambo limefanya Manara awe mtu wa kawaida sana hivi karibuni. Na kwa kujua hilo ameanza kuishi maisha ya porojo za mitandaoni tu. Mara afafanue magoli ya penalty mara propaganda za kumsaini Chama n.k.

Kiufupi, siku hizi hana content kabisa, anavizia matukio Ya Simba ndio apate cha kupost mtandaoni ili jamii ya soka itambue kama yupo. Na tabia hii aliijenga akiwa Simba; alitumia Matukio na mafanikio makubwa ya Simba kujijengea content mitandaoni. Ndio maana alisaini balozi za kutosha.

Kuna wakati unaweza jiuliza Adui wa Manara ni nani kati ya kalabu ya Simba na Uongozi?.

Ukisema ni Timu basi ni bora aache mara moja, hakuna mtu alishindana na taasisi akatoboa. Simba na Yanga zina umri wa zaidi ya miaka 80.

Zilikuwepo kabla hata ya Tanzania kuundwa, zipo leo na zitakuwepo daima, huenda mpaka kiama. Ukiamua kupoteza muda kupambana nazo hadharani, tambua utazeeka na kufa ukiziacha zinapepea. Hata waasisi wao walishageuka rutuba ardhini ila zenyewe zipo.

Ikiwa Ugomvi wake ni viongozi wa Simba basi napo namuhurumia kwa sababu anapambana na watu wanaomzidi hadhi. Mo Dewji anamiliki utajiri wa kiasi cha pesa takribani trilioni 3 za kitanzania. Je, Manara akizichanga mali zake zote anaweza.

Credit: East African Soccer ZONE

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

1 Comments

  1. Mwehu kashuka sana hana deals zozote kama alivyokuwa Simba ndo ajue Simba ni big brand

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)