Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Harmonize Atamba "Hakuna Msanii wa Kunifikia Bongo"

SUPASTAA wa Bongo Fleva, namzungumzia CEO wa Konde Gang, Harmonize amewatolea uvivu wanaojaribu kumlinganisha yeye na wasanii wengine kwenye industry ya muziki wa Bongo Fleva nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Story yake, Konde Boy ameandika ujumbe unaoonesha kuchukizwa kwake na kitendo hicho kwa maneno yaliyosomeka kama ifuatavyo.

“Unakosea sana kama unanilinganisha na msanii yeyote kwenye kwenye game ya muziki kwa sababu nina “Sound” vizuri kuliko msanii yeyote, ninakoelekea ni kuubadilisha huu mchezo (game ya muziki), ni suala la muda tu, kama umeisikiliza vizuri album ya ‘High School’ natumani utakuwa unaelewa ninacho kizungumzia.

“Ninafanya hivi kwa ajili ya kizazi kipya, kama ushazeeka, ushapitwa na wakati huwezi kuupenda muziki wangu. Namaanisha kama una miaka kuanzia hamsini huwezi kuuelewa muziki wangu hata kidogo,” ameandika Harmonize.

Harmonize kwa sasa bado yuko nchini Marekani kwa ziara maalum ya kimuziki katika majimbo kadhaa nchini humo, huku albamu yake mpya ‘High School’ aliyoiachia Novemba 5, 2021 ikiendelea kufanya vizuri kwenye platforms mbalimbali za muziki duniani.

Je ni kweli Harmonize ndo msanii bora zaidi Tanzania?🤔✍️


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments