Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ibenge Afunguka Kumweka Benchi Chama


KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, amefunguka suala la kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama, kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho huku akiweka wazi kuwa mchezaji huyo anahitaji muda zaidi wa kukaa sawa ndani ya timu hiyo.


Chama alijiunga na RS Berkane mwanzo wa msimu huu akitokea Simba sambamba na winga wa zamani
wa Yanga, Tuisila Kisinda.


Akizungumza na Global Publishers, Ibenge alisema kuwa suala la Chama kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya timu hiyo inatokana na mchezaji huyo kushindwa kuendana haraka na mazingira ya timu
jambo ambalo linahitaji muda kidogo kwa mchezaji huyo kukaa sawa.


“Chama kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara inatokea kwa wachezaji wengi wakubwa
duniani ambao baada ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine wanashindwa kuendana na mazingira
ya timu haraka jambo ambalo baadaye hubadilika baada ya kuyazoea mazingira, ni kama tu ilivyotokea kwa Chama.


“Hivyo Chama anahitaji muda wa kuyazoea mazingira ya timu ambayo ni mpya kwake, naamini atakuja
kukaa sawa, Chama ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kucheza timu yoyote barani Afrika, hivyo ndio
maana hata sisi tulimsajili, naamini kila kitu kitakuwa sawa huko mbeleni, ni jambo la muda tu,” alisema kocha
huyo.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments