Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Jinsi Vanessa Mdee Alivyomkwapua Juma Jux Mara Baada ya Jack Cliff Kufungwa Jela


Vanessamdee alimkwapua @juma_jux kutoka kwa Jack Cliff, mara baada ya Jack kufungwa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini China. Vanessa Mdee ‘V-Money’ aliibuka na kumzungumzia Ex huyo wa Jux.

Awali, wanahabari walianza kumuuliza kama alikuwa akimfahamu Jack tangu alipokuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Jux ambapo Vanessa alijibu kuwa alikuwa hamfahamu.

“Jack nilikuwa sifahamiani naye. Nilikua namjua tu ni msichana anayefanya music video na nilikuwa naona kazi zake za umodo,” alisema Vanessa kwa kujiamini.

Alipoulizwa anazungumziaje kama endapo Jack atakuwa anaumia kule gerezani anaposikia amekwapuliwa bwana wake (Jux) na pengine haoni kama anamuongezea machungu, Vanessa alifunguka:

“Kwanza kabisa sijamchukulia bwana wake. Namuombea atoke mapema. Ninachoweza kusema, namuombea atoke jela mapema. Matatizo anayoyapata kule ni makubwa kuliko haya ambayo anafikiria. I don’t think she even think about me at all (sifikirii kama ananifikiria mimi kabisa). Nadhani anawafikiria familia yake na hali ambayo amefungiwa pale. Sidhani kama hata ananiwaza.”

Jack alikamatwa Desemba 19, 2013 akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guandong Kusini mwa China.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments