Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Katibu Mkuu CCM Atoa Siku 43 Stendi Chato Kukamilika
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa siku 43 kuanzia leo kwa mkandarasi wa ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ya Kahumu Wilaya ya Chato Mkoani Geita kukamilisha ujenzi ili wananchi waanze kutumia na Serikali kupata mapato.


“Hii stendi ina habari ndefu lakini pia kukamilika kweke hakuna sababu ya kuongezewa muda zaidi, tarehe 30 mwezi wa 12 iwe imekamilika ili serikali iendelee na shughuli nyingine na CCM waweke tiki kuwa wamemaliza kama walivyoahidi na waangalie mengine,” amesema.Ujenzi wa  stendi hiyo ulianza mwezi Februari mwaka 2019 na kutakiwa kukamilika mwezi wa saba mwaka 2020 lakini mpaka sasa utekelezaji wake unasuasua.Mkurungezi Mtendaji wa Wilaya ya Chato Mandia Kihiyo alimwambia Chongolo kuwa ujenzi wake ulipangwa kukamilika mwezi Julai  mwaka 2020 lakin kutokana na sababu mablimbali mradi huo umeshindwa kukamilika na sasa umepangwa kukamilika tarehe 30 mwezi wa kwanza mwaka 2022.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments