Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kocha Mpya kutoa hatma ya nyota hawa Man Utd

 


Vyanzo vya kuaminika nchini England, vimeripoti kuwa, baadhi ya wachezaji watano wa Manchester United wataamua au kuamuliwa hatma yao kocha mpya wa kikosi hicho akipatikana.

Taarifa hizo zimekuja baada ya Manchester United kumtimua kazi aliyekuwa kicha wake, Ole Gunnar Solskjear na mikoba yake kushikiliwa na Michael Carrick kwa muda.

Wachezaji hao ambao mpaka sasa hawajui hatma yao klabu hapo ni, kiungo Don Van de Beek, kipa Dean Henderson, winga Anthony Martial, mabeki Erick Bailly, Alex Telles na Diogo Dalot ambao hawakuwa wanapata nafasi sana chini ya Ole.

Mbali na wachezaji hao, Winga Jesse Lingaard ameshaweka wazi maamuzi yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya kushindwa kufikia muafaka kwenye mazungumzo ya kumuongeza kandarasi mpya yaliyofanyika wiki iliyopita.

Manchester United inahusishwa kwa ukaribu na makocha, Brendan Rodgers wa Leicester City ya England, Maurccio Pochettino wa PSG ya Ufaransa na kocha wa zamanai wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye hana timu kwasasa.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments