Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kocha Pablo Awaangukia Mashabiki Simba SC


Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Mhispania Franco Pablo Martin amesema anawashukuru sana mashabiki wa Simba kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo uliopita lakini anawaomba waje kwa wingi kwenye mchezo ujao.

Pablo amesema: “Nawashukuru sana mashabiki waliojitokeza kwa wingi sana kule Mwanza, naamini watakuja kunikaribisha kwa wingi Jumapili wakiwa na jezi nyekundu uwanja mzima,” amesema Kocha Pablo.

Akizungumzia mchezo wenyewe dhidi ya Red Arrows, Pablo utakaochezwa Novemba 28, 2021 amesema utakuwa mgumu na tunapaswa kucheza kwa kujitoa asilimia 100 katika muda wote wa dakika 90 ili kupata ushindi nyumbani.

“Mechi itakuwa ngumu, tupo nyumbani inatupasa kujituma kwa asilimia 100 muda wote wa mchezo ili tupate ushindi. Maandalizi yanaendelea vizuri na matarajio yetu ni kupata ushindi,” amesema Pablo.

Kama Simba ikifanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo basi watalazimika kwenda kucheza ugenini na kuulinda ushindi huo ili watinge hatua ya makundi y michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments