Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kusah: Aunt Ezekiel Ameibeba Roho Yangu

MSANII wa Bongo Fleva, Salmin Hoza almaarufu Kusah anasema kuwa, kwa maisha yake ambayo ameyaishi yapata miaka miwili sasa na mzazi mwenzake ambaye ni staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel hadi hapo alipofikia ni kama anatembea tu na mwili, lakini roho yake ameibeba mzazi mwenzake huyo.

 

Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA, Kusah anayetamba na Wimbo wa I Wish anasema kuwa, siku zote mtu anaweza kupita huku na kule, lakini akajikuta anakwama sehemu moja tu na kubanduka ikawa ni shida sana.

 

Kusah anasema hivyo ndivyo ilivyotokea kwake kwani baada ya kupita huku na kule, sasa amenasa kwa Aunt na anahisi kabisa mwanamama huyo anatembea na moyo wake.

 

“Watu hawajui tu, lakini ukweli hata Mama Nono (Aunt), nahisi anatembea kabisa na moyo wangu. Binafsi naona hilo wazi maana sifikirii kama naweza kupiga hatua yoyote au kubanduka kwake kwenda popote kwani kama ni nanga ndiyo imefika na sasa kama kuna watu wana mpango wa kusubiri tuachane, watangoja sana,” anasema Kusah ambaye amezaa mtoto mmoja na Aunt na kabla ya hapo alizaa na msanii Ruby.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments