Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kwa sheria ya Tanzania, Mtu Ukisafirisha au Kukutwa na Dawa za Kulevya ikiwemo Bangi au Mirungi Kifungo Cha Maisha Jela


#UNAAMBIWA: Kwa sheria ya Tanzania, Mtu ukisafirisha au kukutwa na dawa za kulevya ikiwemo bangi au mirungi (dawa za mashambani) zaidi ya kilo 50, Heroin au Cocaine (dawa za viwandani) zaidi ya gramu 200, kemikali bashirifu zaidi ya kilo 100 au lita 100, ukikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha maisha jela na kosa hili halina dhamana.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015 ambayo ilianza kutumika kuanzia Mwezi September 2015 na kurejewa mwaka 2019. #MillardAyoUNAAMBIWA

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments