Maaskofu wa KKKT Shoo, Malasusa wafikishwa kortini




VIONGOZI wawili wa madhehebu ya Kikristo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa hilo, Dk Alex Malasusa, wameburuzwa mahakamani, wakituhumiwa kuchochea mgogoro katika Dayosisi ya Konde, Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka Mbeya na makao makuu ya KKKT, Arusha zinasema, aliyemburuza mahakamani Askofu Shoo, Dk Malasusa na Bodi ya Wadhamini ya KKKT, ni muumini wa Kanisa hilo, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Dayosisi ya Konde, Alfred Kanyaki.

Viongozi hao wawili na wajumbe wengine tisa wa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa hilo, wamefunguliwa mashitaka hayo, wakituhumiwa kutaka kumng’oa Askofu wa Dayosisi ya Konde, Dk Edward Mwaikali, kinyume cha Katiba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad