Ticker

6/recent/ticker-posts

Madanguro ya Kufanyia Biashara ya Ngono Tanga marufuku.

 

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amepiga marufuku biashara ya Madada Poa ambayo inafanyika katika madanguro maeneo tofauti jijini humo.

Mgandilwa ametoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga na kuagiza Jeshi la Polisi kusimamia suala hilo mpaka likome.

Ameyataja meneo hayo kuwa ni Sabasaba na Barabara ya Uhuru na kuongeza kuwa wanaofanya biashara hiyo maeneo hayo watafute sehemu nyingine.

“Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna madanguro ambayo dada zetu wanajiuza, naomba nitumie hadhara hii kwa kuwa kuna vyombo vya dola, tuanze kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakua msafi” amesema Mgandilwa.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments