Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Majizzo "Sio Davido Aliyembeba Diamond Platnumz Bali Davido Ndio Alibebwa, Wasanii Wawe Makini na Collabo za nje"

Akiwa kwenye Empire ya EFM hii leo tarehe 18/11 mahususi kwaajili ya kuzindua Concert ya Komaa itayofanyika December 4 viwanja vya Tanganyika Peakers, Mkurugenzi wa Efm na TV E, @majizzo ameongelea pia suala la namna Djs na baadhi ya watu wanaotumikia hii sanaa kuua muziki wa Bongo Flava.

Hii inakuwa ni muendelezo wa kile kinacho onekana wasanii wa ndani kutopewa kipaumbele kwenye show zinazoandaliwa na promoters wa Bongo kama inavyo fanywa na wasanii tokea nje.

Pia akitaka watu wajitafakari na neno KIMATAIFA akitolea mfano wa collabo ya @davido na @diamondplatnumz ,My Number One, ambapo amesema kuna mitazamo hasi kuwa Davido ndiye alimbeba Diamond kwenye collabo hiyo, lakini haiangaliwi kuwa Diamond ndiye aliyembeba Davido. Akiuliza ni Show ngapi Davido amefanya Tanzania baada ya Collabo na Diamond,then jiulize ni Show Ngapi Diamond amefanya nchini Nigeria baada ya collabo na Davido.

Ifike hatua wasanii wajue hizi wanazoita international Collabo ndizo zinapelekea hadi pesa zao kubebwa na hao washirikishwaji,hivyo zinapaswa kuwa na faida pande zote mbili.

Pia ametolea mfano wa collabo ya @marioo na Shomadjoz, Mama Amina ni wimbo mkali aliopewa shavu jozyy, Marioo akijichanga hadi kushoot video SA, ila hadi wimbo unapoa, simu za Show haziiti kivile kwa Marioo, Shomadjoz kaja baada ya hiyo Collabo kala show kibao na kuondoka na mkwanja wa kitanzania ambao si chini ya 40M+.

Internationallyđź’”

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments