Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Makamba: Hakuna Uhaba wa Mafuta, Bosi TPDC Ajieleze


WAZIRI wa Nishati January Makamba, amesema Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, Dkt. James Makaragio, atafika ofisini kwake kwa ajili ya kutolea maelezo kauli yake aliyosema kwamba kama meli ya mafuta haitoingia nchini ndani ya siku 15 basi kutakuwa na uhaba wa mafuta.

 

Waziri Makamba ameyaeleza hayo, kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kwamba hakuna uhaba wa mafuta nchini na wala hakuna haja ya kuzua taharuki kuhusu upatikanaji wa nishati hiyo na kwamba serikali inaendelea kuchukua hatua ili kuongeza uhakika wa upatikanaji wake na unafuu wa bei.

 

Akijibu swali la mdau alieuliza mkanganyiko kati ya mkurugenzi wa TPDC na kauli yake kujichanganya, Makamba amesema yake ni Kauli ya uhakika ya Serikali.

 

“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei.

 

“Kauli ya uhakika ni ya serikali, Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika, pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada,” ameandika Waziri Makamba.

 

Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake kwasababu aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia amemtaka mkurugenzi wa TPDC aende ofisini kutoa maelezo kabla hajachukuliwa hatua za ziada.


 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

Post a Comment

0 Comments