Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mamilioni ya Fedha Yalitumwa kwa Washirika wa Joseph Kabila
Kampuni zinazomilikiwa na familia na marafiki wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila zilitumiwa mamilioni ya dola za fedha za umma kupitia akaunti zao za benki, kulingana na uvujaji mkubwa zaidi wa data barani Afrika.


Pesa hizo zilihamishiwa kwenye akaunti za kampuni hizo katika benki ya BGFI ya Congo, Mamilioni ya pesa taslimu kisha yalitolewa kwenye akaunti.Bw Kabila alikuwa rais wakati wa uhamisho wa fedha hizo kupitia benki, Amekataa kujibu maswali yetu kuhusu uhamisho huo.Uvujaji huo ulijumuisha zaidi ya hati milioni tatu na taarifa kuhusu mamilioni ya miamala kutoka kwa benki ya BGFI (Banque Gabonaise et Française Internationale), ambayo inahudumu katika nchi kadhaa za Afrika na Ufaransa. Jarida la upelelezi la Ufaransa la mtandaoni Mediapart na Jukwaa lisilo la Kiserikali la Kulinda Watoa taarifa katika Afrika (PPLAAF) zilipata taarifa hizo.BBC Africa Eye iliweza kupata ushahidi huo, kama sehemu ya muungano uitwao Congo Hold-up, unaoratibiwa na mtandao wa vyombo vya habari wa European Investigative Collaborations (EIC).Uchunguzi huo unazua maswali kuhusu ni nani aliyenufaika kutokana na uhamisho wa fedha na uwezekano wa migongano ya maslahi.Kampuni ya mafuta isiyokuwa na mafuta

Mkurugenzi mkuu wa kampuni tanzu ya BGFI ya DR Congo, BGFI Banque RDC, kutoka 2012 hadi 2018 alikuwa Francis Selemani, kaka wa kambo wa Joseph Kabila.Dadake Bw Kabila, Gloria Mteyu, alimiliki 40% ya operesheni ya BGFI DR Congo, iliyoanzishwa mwaka wa 2010.Kampuni moja ya kibinafsi, Sud Oil, ilionyeshwa kupokea karibu $86m katika fedha za umma kuanzia Novemba 2013 hadi Agosti 2017.Hizi ni pamoja na angalau $46m kutoka kwa mdhibiti wa benki wa DR Congo, BCC, $15m kutoka kwa kampuni ya uchimbaji madini ya serikali ya GĂ©camines, na $1.3m kutoka tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, Ceni.

Taarifa pekee ambayo BBC ilipata kutokana na uvujaji wa malipo haya ilikuwa hati ya malipo ya zaidi ya $1m kutoka Ceni hadi Sud Oil kwa bidhaa za petroli.BBC haikupata ushahidi wowote kwamba Sud Oil ilikuwa ikiuza bidhaa za petroli wakati huo.Mke wa Selemani, Aneth Lutale, alikuwa na umiliki wa asilimia 80 wa Sud Oil na Bi Mteyu alimiliki asilimia 20 iliyobaki kuanzia 2013 hadi 2018.Mamilioni ya dola yalihamishwa kutoka akaunti za BGFI za Sud Oil hadi akaunti za kampuni nyingine za kibinafsi za BGFI. Baadhi ya hizi zilimilikiwa na jamaa au wafanyabiashara washirika wa Bw Kabila, ambaye alikuwa rais kutoka 2001-2019.Moja ya makampuni haya, Kwanza Capital, ilikuwa inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na mfanyabiashara Mkongo Pascal Kinduelo, huku Sud Oil ikichukua hisa chache. Bw Kinduelo alikuwa mwenyekiti wa BGFI Bank RDC wakati huo.Bw Kinduelo pia alikuwa mmiliki wa zamani wa Sud Oil, kabla ya kuhamisha umiliki.Uchunguzi uligundua benki hiyo iliruhusu utoaji wa pesa nyingi za thamani ya juu kutoka kwa akaunti ya Sud Oil, ikijumuisha moja ya $ 6 milioni. Kwa mujibu wa sheria kiwango cha juu cha $10,000 kinaruhusiwa kutolewa kwa pesa taslimu kwa siku. Kikomo hiki kinaweza tu kukiukwa kwa madhumuni mahususi, yaliyoandikwa, kama vile sababu za dharura za kitaifa au za ulinzi.BBC Africa Eye haikupata ushahidi katika uvujaji huo kwamba taratibu sahihi zilifuatwa katika matukio haya. Utoaji huu wa pesa taslimu kutoka kwa akaunti ya Sud Oil ulifikia angalau dola milioni 50 kwa kipindi cha miaka minne. Mara pesa hizo zilipotolewa, inaaminika kuwa hazikuweza kujulikana zilikoUkaguzi ulipata kampuni kuwa na 'hatari kubwa sana'

Uchunguzi wetu uliweza kubaini kuwa Sud Oil, kwa kipindi cha 2013 hadi 2018, ilikuwa na mfanyakazi mmoja, mkurugenzi mkuu David Ezekiel, na ofisi ndogo katika mji mkuu Kinshasa kama anwani yake. Mnamo Oktoba 2013, Sud Oil ilinunua mali ya majengo isiyohamishika katika mji mkuu kwa dola milioni 12, na kuweka kampuni hiyo hapo.Pia ilikuwa na mkataba na BGFI Banque RDC kutoa magari mapya kwa wasimamizi wake wakuu kadhaa, akiwemo Bw Selemani. Ilitoza $70,000 kutoa gari lake la four-wheel drive.BBC Africa Eye haikupata ushahidi wa shughuli zozote za biashara.Uchunguzi huo ulipata ripoti ya ukaguzi wa ndani wa BGFI, uliokamilika Julai 2018, ukikosoa vikali operesheni ya DR Congo. Ukaguzi haukusudiwa kuwekwa hadharani.Ilitoa alama ya "hatari kubwa sana" kwa kampuni tanzu ya DR Congo. Pia ilirejelea ukosefu wa uadilifu na uwazi katika kutangaza migongano ya kimaslahi na utekelezaji katika shughuli zake na wateja.Ukaguzi ulimtaja Selemani kuwa na migongano ya kimaslahi isiyopungua 16, ikijumuisha uhusiano na kampuni binafsi zinazomiliki akaunti katika benki hiyo. Pia iliangazia miamala kadhaa ya bei ya juu na Sud Oil.Wiki mbili baada ya ripoti kukamilika, Bw Selemani alihamishwa hadi kwenye nafasi mpya katika ofisi kuu ya BGFI nchini Gabon. Inasemekana alipokea $1.4m alipoondoka BGFI Banque RDC. Anaripotiwa kuondoka BGFI mnamo Novemba 2018.Sud Oil ilibadilisha umiliki mnamo 2018 na Kwanza Capital ilifungwa mwaka huo huo. Bi Mteyu anafahamika kuwa alitoa 40% ya hisa zake katika BGFI Banque RDC.BBC Africa Eye iliwasiliana na BGFI, Joseph Kabila, Francis Selemani, Aneth Lutale, David Ezekiel na Gloria Mteyu juu ya taarifa zilizomo kwenye uvujaji huo. Hakuna aliyejibu maswali yetu. Pia tuliwasiliana na Pascal Kinduelo, ambaye alikataa kujibu.Gecamines na BCC hawakujibu maombi ya BBC ya kujibu.Mkuu wa Ceni wakati wa shughuli zake na Sud Oil, Corneille Nangaa, alikataa kutoa maoni yake kuhusu malipo hayo, akitoa sababu za sheria za usiri za bunge. Bw Nangaaa aliongeza kuwa timu mpya ya usimamizi sasa inaendesha tume ya uchaguzi.Uchunguzi wa BBC Africa Eye utapatikana mtandaoni kutazamwa kuanzia tarehe 29 Novemba.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments