Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mkuu wa idara ya Jinai Kenya George Kinoti ahukumiwa kifungo cha miezi 4 jela kwa kukaidi mahakama
Mkurugenzi wa idara DCI nchini Kenya George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kukosa kutii agizo la mahakama lililomtaka kuachilia bunduki za mfanyabiashara Jimi Wanjigi.


Kinoti anatakiwa kujisalimisha gerezani ndani ya siku saba la sivyo Inspekta mkuu wa Polisi kutekeleza hati ya kumkamata.Jaji wa Mahakama ya Kuu Anthony Mrima mnamo Januari 2019 aliamuru DCI, Inspekta mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma kurejesha bunduki na risasi zote zilizochukuliwa kutoka kwa makazi ya Wanjigi mnamo 2017.Silaha zinazotafutwa ni bastola moja ya ya Smith and Wesson, bastola moja ya Glock, bunduki moja kati ya zingine.Mrima katika kutoa agizo hilo alisema Serikali ilikosea kuchukua bunduki za Wanjigi ilhali bado ana leseni halali.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments